Wakati Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu wa 2021/22 ikielekea ukingoni, Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele anahusishwa na mpango wa kuachana na klabu hiyo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kisoka na kuzifumania nyavu za timu pinzani.
Mayele ambaye amefunga zaidi ya mabao 10 katika ligi hiyo, anahusishwa na mpango wa kuwaniwa na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika RS Berkane, chini ya Kocha Mkuu Florent Ibenge.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari kutoka Congo DR vimethibitisha kuwa, Kocha Ibenge ambaye aliwahi kufanya kazi na Mayele katika klabu ya AS Vita, amevutiwa na uwezo wa Mshambuliaji huyo baada ya kumfuatilia kwa ukaribu akiwa Young Africans msimu huu 2021/22

0 Comments